Saturday 4 June 2016

Sarafu za Valorbit za Bure - (Free Valorbit Coins)

CRYPTOCURRENCY NI NINI?
Cryptocurrency ni aina ya fedha ya kidigitali (digital money/digital currency) ambayo haihusiani na nchi yeyote. Pesa hizi huhifadhiwa na kutumika kwa kupitia mtandao wa kompyuta tu. Hazina noti wala sarafu. Unaweza kuilinganisha na pesa uliyoweka katika akaunti yako ya M-Pesa ambayo unaweza kuitumia kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kwa kutumia simu yako ya mkononi.  Cryptocurrency huhifadhiwa kwenye akaunti ziitwazo wallet (mkoba) ambayo unaweza kuilinganisha pia na akaunti yako ya M-Pesa. Wallet ina mchanganyiko wa namba na herufi nyingi mfano 1MCnQsTHfirvZ8Yx46g1kB94D3qo3hymdZ.
Katika cryptocurrency ziko fedha au sarafu zenye majina mbalimbali. Fedha ya kwnza ya aina hii ilikuwa Bitcoin (BTC) iliyoanzishwa mwaka 2009. Baadae zilikuja pesa zingine zikiiga mfumo wa Bitcoin. Baadhi ya pesa hizo na alama (symbol) zake ni hizi:

Litecoin (LTC), Dogecoin (DOGE), Ethereum (ETH), FeatherCoin (FTC), Namecoin(NMC) n.k.
Yapo mamia ya cryptocurrency.
Valorbit (VAL): Sarafu hii imeanzishwa Januari,2016. Tofauti na sarafu nyingine za aina hii, waanzilishi (developers) wa sarafu hii wameamua kugawa kiasi kikubwa cha sarafu hii bure kwa mtu yeyote duniani kupitia mtandao wa Facebook au kwa njia ya email. Mtu yeyote anaweza kupata mwaliko wa kujipatia kuanzia sarafu 1000 za Valorbit (VAL).
Kabla hatujaendelea kujifunza zaidi kuhusu VAL na cryptocurrency kwa ujumla, ninakualika utembelee ukurasa ufuatao hapo chini ili ujipatie sarafu zako bure halafu tutaendelea kuona namna gani sarafu hizi zinaweza kuwa na thamani kubwa baadae.
Tembelea mwaliko huu na ujiunge kwa kupitia akaunti yako ya facebook. Ukishafungua ukurasa huo bofya mahali palipoandikwa CONNECT WITH FACEBOOK.

https://valorbit.com/signup/OM0Nffnlglq8VTBQavviqg

THAMANI YA SARAFU ZA KIDIGITALI
Thamani ya sarafu ya kidigitali hutegemea sana idadi ya watu wanaoikubali au kuitumia (community support) na matumizi yake katika ulimwengu halisi (real world applications). Sarafu kama Bitcoin ilipoanzishwa mwaka 2009 ilikuwa na thamani ya senti kumi za dola ya Marekani ($0.10) ambayo ni kama shilingi 220 hivi za Kitanzania. Miaka mitano baadae Bitcoin ilikuwa imefikia thamani ya zaidi ya dola 1000 za Marekani, yaani zaidi ya  shilingi 2,000,000 za kitanzania. Wale waliokuwa wamenunua bitcoin zilipoanza walikuja kuziuza baadae kwa faida ya ajabu.
Bitcoin imegawanywa kwenye sehemu ndogondogo ziitwazo satoshi. Bitcoin moja in satoshi milioni mia moja (100,000,000). Satoshi moja huandikwa hivi:  0.00000001 BTC

 MATUMIZI YA SARAFU ZA KIDIGITALI (Cryptocurrency)
 Bitcoin imekubalika sana na unaweza kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali mtandaoni na ukalipia kwa Bitcoin kwenye maduka mengi yanayoipokea kama njia ya malipo pote duniani. Kwa hapa Tanzania unaweza kununua muda wa maongezi wa simu yako kwa kutumia bitcoin kwenye mitandao kama www.piiko.com, www.xapo.com, www.bitmoby.com na bitrefill .com. Thamani ya cryptocurrency hupanda na kushuka kama ilivyo kwa fedha za kawaida. Fedha za kawaida tunazotumia huitwa fiat currency. hizi za kidigitali zinzitwa cryptocurrency kwa sababu zimebuniwa kwa teknolojia ijulikanayo kama cryptography.Leo thamani ya bitcoin moja ni kiasi cha dola 450, karibu sawa na shilingi milioni moja za kitanzania.Si sarafu zote zilizopata mafanikio makubwa na kukubalika kama Bitcoin. Zipo sarafu nyingi zilikuja na zikapotea baada ya muda mfupi kutokana na kukosa idadi ya kutosha ya watu wa kuiunga mkono. Jamii ni muhimu sana kwa mafanikio. Pia unaweza kubadili bitcoin na kupata pesa za kitanzania kwa njia ya M-Pesa kupitia kampuni ya Bitpesa  , www.bitpesa.co.
Sarafu zingine kama Litecoin(LTC) na Dogecoin (DOGE) pia zimepata mafanikio ya kutosha japo hazijapanda thamani kwa kasi kama Bitcoin. Blog hii ni maalum kwa sarafu ya Valorbit (VAL) kwa hiyo itajikita zaidi huko.

UPATIKANAJI WA SARAFU ZA KIDIGITALI 

Zipo njia kadhaa unazoweza kutumia kujipatia sarafu hizi ila kwa sababu blog yangu inalenga kumuelimisha mtu asiye na uelewa wowote wa masuala  ya cryptocurrency, nitaepuka mambo yaliyo ya kitaalamu kwa wakati huu ni kuongelea yale ambayo ni rahisi kueleweka na wote. Baadhi ya njia za kujipatia sarafu za kidigitali ni:
  • Kununua mtandaoni kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kidigitali yanayojulikana kwa kiingereza kama cryptocurrency exchange. Mfano wa maduka hayo ni www.c-cex.com, www.bittrex.com,www.yobit.net, www.poloniex.com. 
  • Kufanya kazi kupitia mtandao na kulipwa kwa bitcoin. 
  • Kupata vipande vidogo vidogo vya sarafu kwa kutembelea tovuti ziitwazo faucet.
  • Kupata sarafu za bure kama ilivyo kwa Valorbit ambapo waanzilishi wake wanatumia njia hiyo kuifanya sarafu iweze kujulikana na kuenea kila mahali. Valorbit ndiyo sarafu pekee ambayo imegawiwa bure kwa watu wote duniani kwa mabilioni ya sarafu.

NIA YA BLOG HII

Kwa nini nianzishe blog ya kuwaonyesha watu namna ya kupata sarafu hizi bure? Labda mtu anaweza kusema ninayo ajenda ya siri nyuma yangu. Sababu yangu ni hii. Mimi ni mhamasishaji wa cryptocurrency na kwa kuhamasisha watu wapate Valorbit za bure nasaidia kukuza thamani ya VAL na hivyo kwa kuwa mimi mwenyewe namiliki sarafu hizi ambazo nimezipata kwa kualikwa kama nilivyokualika wewe na pia kwa kuzinunua, kadiri jitihada zangu zinavyoipandisha VAL thamani ndivyo na uwekezaji wangu unavyoongezeka thamani. Kwa sasa VAL haina thamani kubwa. VAL moja ni sawa na satoshi moja ya Bitcoin ambayo ni kama senti moja ya shilingi. Mgao wa bure wa VAL utafikia kikomo muda si mrefu na hapo ndipo VAL itakapopanda thamani na endapo VAL moja itafikia angalau thamani ya shilingi moja ya kitanzania basi wale watakaokuwa wamejikusanyia VAL za kutosha watakuwa wenye furaha isiyo kifani. Wataweza kuiuza kwenye exchange kwa bei nzuri. Kwa sasa VAL imeingia kwenye soko (exchange) la Yobit (www.yobit.net).